Mwanakikundi zuhura Mnandembwe akitoa maelezo ya namna alivyohamasika na kujiunga na chf mbele ya wananchi waliopo katika kata ya Kilangala,amewataka wananchi wasio kwenye sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huu kwani ni mkombozi wa huduma za matibabu nchini,ukizingatia wengi ni wenye vipato vya wastani na visivyo vya uhakika.
Mwananchi wa kata ya Mihumbwe Sharifa Mzee kushoto akipata ufafanuzi wa namna ya kujiunga na mifuko ya afya ya jamii (CHF) kutoka kwa msimamizi wa NHIF na CHF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond baada ya kuhamasika kwenye viwanja vya chama cha msingi cha ushirika (AMCOS) Kilangala.
Alamski
Wanakikundi wa WAMA kata ya kilangala wakijiandikisha kwenye mfuko wa afya ya jamii (CHF),anayeandikisha kulia ni msimamizi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya lindi fortunata raymond,kushoto ni Mganga mfawidhi wa kata hiyo Dr. Arafa Abdallah,takribani kaya 105 zilijiunga papo kwa papo ,uandikishajii huo ulifanyika kwenye viwanja vya chama cha msingi cha mazao (AMCOS) Kilangara Mkoani Lindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...