Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimimbili Dkt. Marina Njelekela amewaagiza wafanyakazi wa Hospitali hiyo kutafuta mbinu mbalimbali za kuongeza mapato, kupunguza matumizi na kuziba mianya ya upotevu wa mapato. Dkt. Njelekela ametoa agizo hilo leo alipokuwa akifunga Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi hao uliofanyika katika Hoteli ya Landmark iliyoko Jijini Dar Es Salaam.
Description: DSC07539
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela hayupo pichani

“Ninawaagiza Wakurugenzi, Wakuu wa Idara, Wakuu wa Vitengo, Mameneja wa Majengo mlioko hapa leo kushirikisha wafanyakazi walioko chini yenu ngazi zote ili kuja na mikakati, mbinu za kubuni vyanzo vipya vya mapato katika maeneo yenu ya kazi, kutoa maoni yenu ni wapi mnafikiri kuna matumizi zaidi ili yapunguzwe na pia ni wapi mnaona kuna mianya ya upotevu wa mapato ya Hospitali ili tuweze kushirikiana kuziba mianya hiyo” amesema Dkt. Njelekela.


Amesema kuwa ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kupanga, kutekeleza shughuli mbalimbali za Hospitali ni muhimu kwani unatoa fursa kwa wafanyakazi kujua Hospitali inafanya nini, kwa wakati gani, nani anayepaswa kufanya nini, kwa kutumia mbinu gani na rasilimali gani zipi na kiasi  gani zitahitajika ili kufanya kazi hiyo.

Kwa sasa tunamalizia mpango wetu wa kazi kwa robo ya kwanza ya mwaka kwa misingi hiyo natoa mwezi mmoja wa Oktoba kuhakikisha maagizo niliyotoa yanatekelezwa ili kutoa nafasi ya mapendekezo, mbinu, mikakati yenu kufanyiwa kazi vizuri katika robo ya pili na ya tatu ya mwaka wa fedha 2013/2014, alisisitiza Dkt. Njelekela.
Fuatilia habari zaidi katika picha zifuatazo;
Description: DSC07529
Description: DSC07520
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela hayupo pichani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...