Staa wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo,Rehema Chalamilla 'Ray C', akiingiza sauti ndani ya Studio za THT, chini ya maprodyuza Emma The Boy na Tudy Thomas,ambao wamepania kumrejesha katika game kwa kishindo msanii huyo, ambaye alipotea kwenye ulimwengu wa Burudani baada ya kutopea katika utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa sasa ameachana nayo na kumrudia mwenyezi Mungu sambamba na kuendelea kutumia dozi ya kuondoa sumu ya madawa hayo.
 Prodyuza  Tudy Thomas (kulia), akijadiliana jambo lililotokana na majadiliano ya kuboresha ngoma mpya ya Ray C, pichani kati ni  Emma The Boy akipiga mzigo tayari kwa kumkamilishia Ray C ngoma yake mpya ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.
 Ray C, akijaribu kutoa akapela kwa Maprodyuza hao, wakati wakiendelea kuiboresha ngoma yake mpya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. uzito wa kuangaliwa. Mtu ni afya.

    ReplyDelete
  2. Ingependeza kama ungerudi kwa nyimbo za gospel, nadhani ungefanikiwa zaidi sio tu kwa kutuburudisha bali kumsifu mungu pia katikammambo uliyopitia. Hizi bongo fleva waachie watotonhazikufai kwa sasa. Na haitapendeza kukuona tena jukwaani ukikata viuno. Ni wazo tu...

    ReplyDelete
  3. Kila mtu kimpango wake bwana..dont frustrate her efforts..
    Kila mtu na wito wake. Mwacheni miaka mia mbona Tshala mwana Mbilia Bel,Yondo sista, Tina Turner hamkuwashauri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...