Hadi sasa watu wapatao 45 wamepoteza maisha kwa mafuriko yaliyosabishwa na kimbunga sehemu zilizo mwambao wa bahari hasa sehemu maarufu ya utalii Acapulco.
Nyumba nyingi zimekumbwa na mafuriko.
Uwanja wa ndege na barabara kuu-highway kuelekea Acapulco zimefungwa. Pia hotels nyingi hazina umeme na mawasiliano ya simu, hivyo watu wengi walioenda kwa mapumziko hawana masiliano na familia zao.
Wakazi wa Acapulco wana shida ya usafiri kuelekea kazini hasa ukizingatia kuwa barabara zime jaa maji. Hivyo wengi wao wanajaribu kwenda kwa miguu ili kufika kazini ili kuogopa kupoteza ajira zao.
Mimi Joseph Machele na wenzangu Epimaki Ngowi , Moshy Kalangula , Nyabenda Mporakumugero, Seif Mohamed Maisi, Samuel Haule , Magobeko Laban Dotto Steven Masilingi na Ombeni Maleo wote tu wazima na familia zetu.
Watanzania tuishio México tupo mbali na bahari yaani sehemu mafuriko yalipotokea. Tafadhari tusaidie kurusha habari hizi kuwandoa hofu ndugu na jamaa.
Nimekuwa nikipata msg nyingi toka Tanzania kutujulia hali, tatizo ni kwamba wasipoweka majina yao sifahamu ni nani katuma sms, make namba za cell phones zinazoonesha zina code za USA.
KIMBUNGA?
ReplyDeleteSio Kimbunga hiki hiki cha Dr. Emmanuel Nchimbi cha Wahamiaji haramu?
POLENI SANA KWA HILO!
ReplyDeleteIla ndugu yangu Joseph Machele,naomba kukutanishwa mmojawapo wa uliyewataja ambaye ni NYABENDA MPORAKUMUGERO na zaidi anaitwa LEONIDAS NGENZEBHUKE NYABENDA MPORAKUMUGERO(A).Ni mjomba wangu.Kwa sasa niko USA katika Jimbo la IOWA kwa masomo tangu 2011.
Nitafurahi.
POLENI TENA KWA MISUKOSUKO,ila tunashukuru kwa taarifa kuwa muko wazima.
email yangu ni:kibambizi@gmail.com.Nitatoa namba yangu ya simu akinitumia Email yake.
Jina langu ni Deo'Gracia Kibambizi wa Kashinga-Rulenge-Ngara-Kagera Tanzania.