AMRI YA RAIS JK KUHUSU WAHAMIAJI HARAMU !

Wananchi washirikishwe katika kuwafichua wahamiaji haramu na kuwa ripoti katika vyombo vya dola !

Katika kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka wahamiaji wote haramu waondoke nchini,kuna haja kubwa ya wananchi kushirikiana vyombo vya dola katika kuwafichua wahamiaji hao haramu ,kwa kuwashirikisha wananchi kazi ya kusafisha maovu na uvunjwaji wa amani unasababishwa na wahamiaji hao itafanikiwa kwa kasi kubwa.

Kama vyombo vya dola vitawashirikisha wananchi na viongozi wa mashina katika serikali za mitaa zoezi hili litafanikiwa kwa haraka sana.

Mkuu wa nchi ambaye ndiye amri jeshi mkuu mwenye majukumu makubwa nchini Rais Dkt.JK kuanzia mwezi Julai 2013 alitoa agizo la siku 14 kwa wahamiaji wote haramu kuondoka nchini au kujisalimisha kwa vyombo vya dola,lakini hadi sasa wahamiaji walioondoka ni wachache na wengi wao bado wanajifaragua mitaani huku vyombo vya dola vikiwatazama.

Kwanini ? agizo hili la Rais JK lisiliwashirikishe wananchi,madiwani,wakuu wa mikoa na wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa . kazi ifanyike kwa haraka. Mungu Ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais JK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. There is no being who is illegal on this planet

    ReplyDelete
  2. Tuko pamoja mkuu. Huwezi ukafanya nchi kama shamba lisilokuwa na mwenyewe. Lazima watanzania tushirikiane kuwafichua watu hawa.

    ReplyDelete
  3. SHERIA IPITISHWE NA SERIKALI KUWA:

    1) Gari/basi la mikoani likikamatwa limebeba wahamiaji haramu - Litaifishwe, pia dereva na konda lupango/jela;

    2) Hotel au gesti itakayokutwa imelaza wahamiaji haramu itaifishwa na serikali pia meneja wa hotel aliyekuwa zamu na mafanyakazi wa mapokezi aliye wapa vyumba - lupango/jela;

    3) Mwenye nyumba aliyewapangisha wahamiaji haramu mfano wasomali, nyumba yake mbezi beach, magomeni, mwananyamala n.k. lupango/jela na pia nyumba hiyo kutaifishwa na serikali.

    4) Mwajiri aliyeajiri wahamiaji haramu lupango/jela.

    5) Wahudumu wa hoteli na gesti house watakaotoa taarifa immigration/polisi kuwa bosi wao kawapangisha kinyemela wahamiaji haramu - zawadi

    6) wafanyakazi wataotoa taarifa bosi wao kaajiri wahamiaji haramu - zawadi

    mdau, alex bura, dar

    ReplyDelete
  4. hahaaa eti "wanajifaragua" umenikumbusha mbali!

    ReplyDelete
  5. Wahamiaji haramu wanawanyim fursa Wazawa licha ya kuwa suala la Wahamiaji lina mitazamo miwili tofauti:

    KIUCHUMI:
    Wahamiaji wanamanufaa kama wataingiza Mitaji na kuhamishia Ujuzi na Tekinolojia nchini kutokea kwao, lakini isiwe wale Wachina wanaokuja kufanya Umachinga ama kuuza Matikiti ambao sisi tunaweza.

    KISIASA:
    Wahamiaji hawatakiwa Kisiasa na ndio maana mivutano inatokea kati ya Wanauchumi na Biashara na Wanasiasa juu wa Wahamiaji nchi zote duniani.

    Lakini kwetu tuwakatae na kama wanakuwepo wawe wenye faida.

    ReplyDelete
  6. Katika Zoezi hili,

    Waulizeni ndugu zetu Ughaibuni waeleze ni kuwa kinacho wakuta Wahamiaji haramu kwa Operesheni Kimbunga ndicho kinawakuta hata ndugu zetu huko walipo.

    La muhimu waelimishwe wasije wakadai wao ni Warundi ama Wanyarwanda ili kupata Ukimbizi kwa kuwa wakurudishwa Rwanda ama Burundi watajulikana sio kwao maana hawana hata ndugu mmoja, na wakiletwa Tanzania watakumbana na ''OPERESHENI KIMBUNGA'' ya Dr. Emmanuel Nchimbi na kurejeshwa Mpakani Rwanda ama Burundi hivyo dunia itakuwa mzigo mzito kwao!!!

    ReplyDelete
  7. Watakao rejeshwa wasijulikani ni wa Tanzania ama Burundi, kwa kujifanya Warundi ili kupewa Ukimbizi watajikuta wakiwa STATE LESS PERSONS kwa muda kama alivyo wahi kuwa Mwanasayansi Albert Einstein kabla ya kupewa Uraia wa Marekani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...