Trela la Lori la Mafuta likiwa limepiga Mweleka katika kijiji cha Kintinku,Wilayani Manyoni Mkoani Singida mapema leo asubuhi mara baada ya kuchomoka kwenye lori hilo na kuacha njia.Kupiga mweleka kwa Trela hilo,kuliwafanya wakazi eneo la jirani na kijiji hicho kuacha shughuli zao na kwenda mbio kwenye ajali hiyo huku wakiwa na madumu makubwa wakiwa na nia ya kuchukua mafuta,kwa bahati nzuri walifika askari Polisi waliokuwa kwenye Doria na kuwakuwa wanakijiji hao wakiwa na madumu yao,hali iliyowapelekea kuwazuia kufanya hivyo na kuweka ulinzi wa kutosha kwenye Trela hilo.
Trela hilo liliwa limezungushiwa Utepe wa njano kuashiria ni hatari katika eneo hilo.
Askari Polisi wa Kituo cha Manyoni wakiwa wamewadhibiti wanakijiji hao pamoja na madumu yao.
Safi sana askari polisi
ReplyDeleteMfano mzuri sana kwa jeshi letu. Polisi ni taasisi ambayo ikifanya uzembe inaonekana mara moja na kinyume chake. Kudos kwa polisi wa kituo hicho.
ReplyDeleteHabari njema kama hii ni kivutio cha biashara na wawekezaji kutoka nje kutumia bandari na kuchagua kuwekeza mitaji nchini kwetu.
Hao wenye madumu ni wananchi au ni wezi watarajiwa? wana dini, dhamiri zao zinawaongoza wafanye nini? Wamemwaga maji wakajaze mafuta ambayo hawakuyapata sasa warejee wakazoe maji ambayo hajakauka kwani kintinku maji shida sana!
ReplyDelete