Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuizindua rasmi shule ya sekondari ya Miono iliyopo Wilayani Bagamoyo, akishuhudiwa na  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe Philipo MulugoRais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Pwani. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maktaba ya Shule ya Sekondari ya Miono Muda mfupi baada ya kuizindua shule hiyo jana Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  wanafunzi wa kidato cha tano wanaosoma Shule ya Sekondari ya Miono Wilayani Bagamoyo, Nyekwabi Jackline George,Penina Odara na Magret Machinyita wakitoa maelezo ya jaribio la sayani somo la biolojia wakati Rais alipofungua rasmi shule hiyo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nchimbi (Waziri wa Utamadauni wa zamani) alikuwa anatafuta vazi la taifa (la kiume); hilo kavaa Rais wetu Kikwete.

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa tarehe 11 (Vazi la taifa ) umenifanya nicheke sana asubuhi subuhi. Mie nilikuwa najiuliza mbona hili shati limekaa tofauti tofauti hivi. Mwenzangu ukanipa jibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...