MWANDISHI wa Habari wa vyombo vya ITV na Radio One, Ufoo Saro (pichani) amepigwa risasi tano maeneo mbali mbali ya mwili wake ikiwemo tumboni, Mbavuni na mguuni na kupelekea kumjeruhiwa vibaya, huku mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro kufariki baada ya kupigwa risasi katika tukio hilo.
Habari ya awali iliyotufikia kwenye dawati letu la habari ndani ya Globu ya Jamii,zinasema kuwa tukio hilo limewahusisha watu wanne ambao ni mwandishi huyo pamoja na mama yake mzazi na mtoto ambao wamefanyiwa kitendo hicho na kijana anayedaiwa kuwa ni mchumba wa Ufoo Saro, ambaye inadaiwa alikuwa nao katika mazungumzo ya kifamilia nyumbani kwao Kibamba jijini la Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa hali ilibaririka mara baada ya kushindwa kuelewana katika mazungumzo yao hayo na ndipo kijana huyo akadaiwa kuwafyatulia risasi na kisha na yeye kujiua kwa risasi.
Baada ya tukio hilo mwandishi Ufoo Saro ambaye hali yake ni mbaya alikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu ya awali na kwa sasa amehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi na kuondolewa risasi zilizomo mwilini mwake.
Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo na tutaendelea kujuzana kadri tutakavyokuwa tunapata taarifa,hivyo tuendelee kuvuta subira.
Jamani mambo gani haya vichaa kupewa bunduki na kuua ovyo ovyo?
ReplyDeletePole sana Ufoo Saro kwa yaliyokufika na familia yako.
Mungu akupe imani na nguvu za kuishi ili kuukabili huu mtihani mgumu uliokufikia.
Mmmh! napinga vikali swala la wananchi kuruhusiwa kumiliki silaha za moto, serikali ichukue hatua ku disarm wananchi wote, la , vitendo hivi vitakuwa vingi, na wengi wataadhirika.
ReplyDeletePole sana Ufosaro, na familia yako. Yaliyo kukuta Ufuosaro hakika ni makubwa mno, hata sijui tukufariji vipi, kupoteza mama, mtoto na mchumba kwa siku moja, na mwenyewe kujeruhiwa namna hiyo. Mungu tu akusaidie, tunakuombea.
Pole sana dada, Mungu ana kila sababu ya kukuponya haraka, ila mtoto wake yupo hai wapendwa
ReplyDelete