Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza na Vijana na wakazi wa Manispaa ya Iringa wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge mkoani Iringa.Wengine ni mbunge wa Iringa (kupitia viti maalum) Mh. Rita Kabati (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Zanzibar Bw.Mohamed Salim Alli.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabrie atembelea banda la maonyesho la WAMATA kuona shughuli zinazotolewa kwa vijana hususan Ushauri nasaha na Upimaji wa Hiari wa Virus vya Ukimwi mjini Iringa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabrie na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Zanzinbar Mohamed Salim Alli (wa tatu kutoka kulia) wakiwa na waongoza midahalo (MC) na shughuli nzima ya Maonyesho ya Wiki ya Vijana katika uwanja wa Mlandege Iringa.
Mbunge wa Iringa Viti Maalum (CCM) Mh. Rita Kabati akiwaasa vijana kuhusu kujinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi katika Uwanja wa Maonyesho wa Mlandege wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Vijana wa Halaiki wakiendelea na maandalizi ya sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Maandalizi ya sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 yakiendelea katika uwanja wa Samora mkoani Iringa leo.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...