Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini somalia wamekamatwa Mkoani morogoro wakiwa wamejificha  katika  lori la mizigo lililosheni chokaa  likitokea jijini dar es salaam kuelekea mkoani mbeya
Kupatikana kwa wahamiaji haramu hao kunatokana na ushirikiano wa  wananchi  ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku wakidai kuwa baadhi yao walikosa hewa kufuatia kujificha katika mizigo hiyo
  Kwa upande wake afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa dereva wa gari hilo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo amesema kuwa  vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa maeneo ya mipaka kwa ajili ya kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu hali inayopelekea wahamiaji hao kutumia njia nyingine ikiwemo ya kujificha katika magari ya mizigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hao madereva wafungwe miaka mingi kwa kubeba raia sehemu ya mizigo na kusababisha vifu vyao...lst time walikufa watu kutoka ethiopia na sasa somalia....inaonekana huyo jamaa hafanani na msomali..lakini wachukuliwe hatua kali sana...wakimbizi warudishwe kwao sio kuwafunga

    ReplyDelete
  2. Huyo dereva na vinara Wa huo mtandao wanastahili kunyongwa. Kuwakaribisha wasomali tena wahamiaji haramu wakati huu ambao hata hatujapona majeraha ya westgate mall ni kuliangamiza taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...