Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau (pichani) amesema kile kinachoonekana kama kushindwa kwa ombi la Umoja wa  Afrika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya yaliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC ni ushindi mkubwa kwa Afrika.

Katika maohjiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la usalama, balozi Macharia amesema Umoja wa Afrika haujakata
tamaa na kwamba wana uhakika wa ushindi dhidi ya ombi lao watakaolipeleka kwenye mkitano maalum the Hague Uholanzi wiki ijayo. Akifafanua kwa msisimko hisia zake kuhusu maamuzi ya baraza la usalama balozi Kamu anaanza kwa kushangaa wanaosema Afrika imeshindwa.

(SAUTI –MAHOJIANO NA BALOZI MACHARIA)
Kusikiliza mahojiano bonyeza hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Balozi Macharia Kamau,

    Inafahamika wazi ya kuwa Afrika ikiwemo nchini Kenya hakukuwa na 'Rule of Law' kitu kilicho pelekea Mauaji na Uhalifu mkubwa dhiudi ya ubinaadamu baadaya Uchaguzi Mkuu 2007/2008.

    Umoja wa Mataifa (UN) umekataa ombi la Afrika kwa kuwa unafahamu fika ya kuwa mtakapo jitoa ktk Mahakama hiyo mtawa jibishwa vipi?, mtawajibishwa na Chombo gani?

    NI USHINDI MKUBWA KWA WANANCHI WA AFRIKA KWA MAAMUZI HAYO YA UMOJA WA MATAIFA!!!

    ReplyDelete
  2. Mnafikiri UN wapo usingizini?

    Ninyi mnafanya Uchaguzi nchini kwenu Kenya mwaka 2007 / 2008 baada ya Matokeo ya Uchaguzi kutangazwa mnachinjana wenywe kwa wenyewe na leo mnataka kujitoa kwenye Mahakama !!!

    ReplyDelete
  3. Maamuzi haya ya Umoja wa Mataifa kukataa maombi yenu Viongozi wa Afrika ni Ushindi mkubwa kwa wananchi wa Kenya na Afrika kwa ujumla!!!

    ReplyDelete
  4. Nimeipenda hii. Ni kweli, ni ushindi mkubwa kwa wananchi wa Kenya na Afrika kwa jumla na si kwa viongozi wao!

    sesophy

    ReplyDelete
  5. Viongozi wenge wa Africa hawazingatii she ria hasa wakati chaguzi mbalimbali ambayo huchangia mauaji ya with wengi undo maana wanataka kuji

    ReplyDelete
  6. Hivi hawa viongozi wa bara Hii Africa wana matatizo gani? saa zote wanajifikiria wao tu, wao wafanye maovu , na hayo maovu wanyatafutia kila mbinu kuyaepuka, wakati watu uhai na mali zo ndio wao wameharibu na kuwaua. Tunapongeza UN kwa msimamo wao sisi kama wafrica wa kawaida, khaki lazima itendeke kwa wote ni sawa

    ReplyDelete
  7. Sponsors wa hiyo resolution was Rwanda and unfortunately record yao congo DRC sio nzuri nina hakika ambae ange sponsor hiyo angetoka nchi yenye heshima kijamii na kimataifa hakika ingepita.

    ReplyDelete
  8. Huu ni ushindi mkubwa kwa people power kwa Watusi wa Africa na pia ningeomba pia UN wapitishe laws za Kuwa Watu wa Africans esp viongozi wote wanaoweka pesa ulaya Kama waoneshi wapepata kihalali basi pesa zichukuliwa ziwe kwenye misaada hapambayo hitasimamiwa na Watu wa nje

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...