Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau (pichani) amesema kile kinachoonekana kama kushindwa kwa ombi la Umoja wa Afrika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya yaliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC ni ushindi mkubwa kwa Afrika.
Katika maohjiano maalum na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la usalama, balozi Macharia amesema Umoja wa Afrika haujakata
tamaa na kwamba wana uhakika wa ushindi dhidi ya ombi lao watakaolipeleka kwenye mkitano maalum the Hague Uholanzi wiki ijayo. Akifafanua kwa msisimko hisia zake kuhusu maamuzi ya baraza la usalama balozi Kamu anaanza kwa kushangaa wanaosema Afrika imeshindwa.
(SAUTI –MAHOJIANO NA BALOZI MACHARIA)
Kusikiliza mahojiano bonyeza hapa
Balozi Macharia Kamau,
ReplyDeleteInafahamika wazi ya kuwa Afrika ikiwemo nchini Kenya hakukuwa na 'Rule of Law' kitu kilicho pelekea Mauaji na Uhalifu mkubwa dhiudi ya ubinaadamu baadaya Uchaguzi Mkuu 2007/2008.
Umoja wa Mataifa (UN) umekataa ombi la Afrika kwa kuwa unafahamu fika ya kuwa mtakapo jitoa ktk Mahakama hiyo mtawa jibishwa vipi?, mtawajibishwa na Chombo gani?
NI USHINDI MKUBWA KWA WANANCHI WA AFRIKA KWA MAAMUZI HAYO YA UMOJA WA MATAIFA!!!
Mnafikiri UN wapo usingizini?
ReplyDeleteNinyi mnafanya Uchaguzi nchini kwenu Kenya mwaka 2007 / 2008 baada ya Matokeo ya Uchaguzi kutangazwa mnachinjana wenywe kwa wenyewe na leo mnataka kujitoa kwenye Mahakama !!!
Maamuzi haya ya Umoja wa Mataifa kukataa maombi yenu Viongozi wa Afrika ni Ushindi mkubwa kwa wananchi wa Kenya na Afrika kwa ujumla!!!
ReplyDeleteNimeipenda hii. Ni kweli, ni ushindi mkubwa kwa wananchi wa Kenya na Afrika kwa jumla na si kwa viongozi wao!
ReplyDeletesesophy
Viongozi wenge wa Africa hawazingatii she ria hasa wakati chaguzi mbalimbali ambayo huchangia mauaji ya with wengi undo maana wanataka kuji
ReplyDeleteHivi hawa viongozi wa bara Hii Africa wana matatizo gani? saa zote wanajifikiria wao tu, wao wafanye maovu , na hayo maovu wanyatafutia kila mbinu kuyaepuka, wakati watu uhai na mali zo ndio wao wameharibu na kuwaua. Tunapongeza UN kwa msimamo wao sisi kama wafrica wa kawaida, khaki lazima itendeke kwa wote ni sawa
ReplyDeleteSponsors wa hiyo resolution was Rwanda and unfortunately record yao congo DRC sio nzuri nina hakika ambae ange sponsor hiyo angetoka nchi yenye heshima kijamii na kimataifa hakika ingepita.
ReplyDeleteHuu ni ushindi mkubwa kwa people power kwa Watusi wa Africa na pia ningeomba pia UN wapitishe laws za Kuwa Watu wa Africans esp viongozi wote wanaoweka pesa ulaya Kama waoneshi wapepata kihalali basi pesa zichukuliwa ziwe kwenye misaada hapambayo hitasimamiwa na Watu wa nje
ReplyDelete