Makamishna wa Bunge pamoja na watu wengine wakiupokea mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Shughuli za Bunge marehemu Anselm Lyatonga Mrema mara ulipowasili nyumbani kwake Marangu Kiraracha tayari kwa mazishi jana.
Mke wa marehemu akiuga mwili wa mume wake aliyefariki tarehe 10/11/2013 mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilillah akiwaongoza watumishi wa Bunge kuuga mwili wa marehemu.
Spika Mstaafu na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta akiweka udongo kaburini kama Ishara ya kumuaga marehemu Anselm Mrema.
Familia ya marehemu Anselm Mrema mara baada ya mazishi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe! (Prosper Minja-Bunge)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. jamani sasa naamini Kaka Mrema hayupo tena.mungu awe mfariji wa familia yake ni ngumu mno jamani kukubali hii hali.RIP A.L.Mrema

    ReplyDelete
  2. RIP. Je huyu ni kaka/mdogo wake Augustine Lyatonga Mrema?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...