Makamishna wa Bunge pamoja na watu wengine wakiupokea mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Shughuli za Bunge marehemu Anselm Lyatonga Mrema mara ulipowasili nyumbani kwake Marangu Kiraracha tayari kwa mazishi jana.
Mke wa marehemu akiuga mwili wa mume wake aliyefariki tarehe 10/11/2013 mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilillah akiwaongoza watumishi wa Bunge kuuga mwili wa marehemu.
Spika Mstaafu na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta akiweka udongo kaburini kama Ishara ya kumuaga marehemu Anselm Mrema.
Familia ya marehemu Anselm Mrema mara baada ya mazishi.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe! (Prosper Minja-Bunge)
jamani sasa naamini Kaka Mrema hayupo tena.mungu awe mfariji wa familia yake ni ngumu mno jamani kukubali hii hali.RIP A.L.Mrema
ReplyDeleteRIP. Je huyu ni kaka/mdogo wake Augustine Lyatonga Mrema?
ReplyDelete