HATIMAYE ile siku iliyokuwa inasubiriwa na wengi, imewadia,
ni GURUMO 53 ndani ya viwanja vya TCC Club, Chang’ombe leo
Jumamosi Disemba 14.
Kama tangazo linavyojionyesha, ni tamasha kubwa la muziki wa
dansi la kustaafu kwa gwiji Muhidin Maalim Gurumo aliyeitumikia
fani hiyo kwa miaka 53 mfululizo.
Gurumo ataimba angalau wimbo mmoja au zaidi wa kila bendi
aliyopitia katika safari yake ndefu kimuziki.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro
Chacha, Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa
ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo
awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo
ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.
Ama kwa hakika ni burudani ya kukata na shoka, bendi kibao,
wasanii kibao – ni burudani mwanzo mwisho kuanzia saa 12 jioni
mpaka majogoo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...