Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,na anaetamba na wimbo mpya wa Facebook,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga.Tamasha hilo ndio kwa mara ya kwanza linafanyika mkoani humo,limezindundiliwa jijini Dar siku ya Krisimasi ndani ya uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watazamaji lukuki.Tamasha hilo baada ya kufanyika mkoani Tanga,kesho litafanyika jijini Arusha na baadae mkoani Dodoma likiwajumuisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

 Pichani kulia ni Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za kusifu na kuabudu kutoka nchini Zambia,Epfrahim Sekeleti akiimba pamoja na mwimbaji mwingine mahiri wa nyimbo injili hapa nchini,Bon Mwaitege pichani shoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...