NA BASHIR NKOROMO
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kikao chake kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete imeibuka na masuala mazito kadhaa, ambayo leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (pichani) ameyaeleza wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam.
Moja ya mambo ambayo Nape amezungumzia, ni kuhusu Kamati Kuu hiyo kuwahoji Mawaziri saba, kujibu kero au mambo kadhaa ambayo yaliibuliwa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana iliyomalizika hivi karibuni katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe.
Nape alisema, Kamati Kuu iliwahoji mmoja baada ya mwingine, kuanzia saa tano asubuhi hadi jioni, baada ya kila mmoja kufika akiwa ameandaa majibu ya tuhuma au hoja alizokuwa ametakiwa kujibu mbele ya Kamati Kuu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...