Mwanafunzi wa Shule ya Msingi katika moja ya Shule za Msingi zilizopo kwenye kijiji cha Ipunga,Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya,akionekana kuvuka daraja la mto unaokatika kwenye Kijiji hicho ambalo limekatika Upande mmoja.hali inayopelekea kuhatarisha usalama wake na usalama wawakazi wa eneo hilo kwa Ujumla.Picha na Mdau Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog.
Home
Unlabelled
HATARI: Mwanafunzi akivuka daraja lililokatika Upande mmoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Jamani. Serikali ya wilaya, lishughulikieni hili tatizo kabla maafa hayajatokea.
ReplyDeleteThat's what we call COMMITMENT!!!
ReplyDeleteHuyo mtoto anafanya zoezi la kuwa Ninja. Ndiyo hali halisi ya Africa, maisha ni kufa na kupona, akifika utu uzima atakuwa amepitia kila challenge ya maisha.
ReplyDeleteSafari ya elimu bure inaanza soon ila vile vile tukumbuke ipo siku utatoa hesabu ya mambo yoote uliofanya duniani
ReplyDeleteDoes the council know that it can be sued if someone loses life? The Council collects taxes and therefore they have an obligation to provide a service/s to the community. Wabongo tuelimishani, kodi zetu siyo za kujaza matumbo yao tu.
ReplyDeleteKodi inayolipwa na waTanzania, hasa wafanyakazi, inatumika wapi????
ReplyDeleteHII NI HATARI SANA KAMA HADI LEO KUNA CHANGAMOTO KAMA HIZI KATIKA VIJIJI VYETU.
HALAFU MNATEGEMEA MTOTO KAMA HUYU AWE NA ROHO NZURI SIKU ZA MBELENI.
ReplyDeleteTUNASUBIRI MSAADA TOKA ULAYA TUTENGENEZE DARAJA; WAHISANI BADO HAWAJAJITOKEZA. ENDELEENI KUTUVUMILIA WANANCHI, HALI SI NZURI YA KIUCHUMI.
ReplyDeleteHii ni Hatari sana. tuwaonee huruma watoto maana ndio taifa la kesho.
ReplyDeleteNa huyo mtoto hana akili. Ina maana haoni kuwa hiyo ni hatari? Kama ameshindwa kujitetea ktk hali hiyo basi huyo taahira
ReplyDeletetatizo anaepita hapo sio huyo mtoto tu, hata wazazi wake na kiongozi wa kijiji wanapita hapo hapo. kwa hiyo sio suala la kusema huyo mtoto hana akili.
ReplyDeletehapo ni mpaka afe mtoto ndo utaona mkuu wa wilaya,mkoa,mbunge,waziri husika hadi rais watakavyo kuwa mahodari kuonge,haya bwana.
ReplyDeleteJAMANI NAONA HAPA MMEKAZANA KUMJADILI HUYU MTOTO, KWANZA NI MTOTO YEYE ANAONA SAWA WALA KWANZA HATA HAJUI SANA HARARI ILIYOPO,SI MNAWAONA WAZEE HAPO PEMBENI WAZEE WAZIMA NA MVI ZAO, WAO WAMELIONAJE SWALA HILO , NA MTOTO ANAPITA NA WANAMUONA
ReplyDelete