Mtaalamu wa Lishe Bi Julita kutoka USAID Tuboreshe Chakula Project akimuelekeza mgeni rasmi katibu tawala wilaya Kongwa, Bw Joseph Kisyela umuhimu na jinsi ya kutumia Virutubishi ambavyo ni muhimu kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5. Sherehe hizo zilifanyika Wilaya Kongwa,kata ngomai mkoani Dodoma 
 Katibu wa wilaya ya Kongwa Bw Joseph Mwita Kisyeli,akitoa hotuba juu ya umuhimu na faida za chakula kilichoongezwa virutubishi,kwa mtoto miezi 6 - miaka 5,katika kampeni ya lishe ilizofanyika kata ngomai wilaya ya Kongwa  chini ya udhamini wa na USAID tuboreshe chakula
 Timu ya watendaji wa serikali wilayani Kongwa.Katibu wa wilaya ya Kongwa Bw Joseph Mwita Kisyeli,wakisiliza  mtaalamu wa masuala ya lishe kutoka USAID Tuboreshe Chakula wakati wa zoezi la kampeni ya kuongeza virutubishi  kwenye chakula linaloendelea wilayani Konga mkoani Dodoma.
 Timu ya wataalamu wa lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Chakula wanaoendesha kampeni ya lishe wilaya mbalimbali za hapa nchini wakiwa  katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa wilaya ya Kongwa Bwana Joseph Kisyeri.
 Baadhi ya kina mama wenyeji wa kijiji cha ngomai,wakishiriki zoezi la kunywesha watoto kampeni za lishe bora zinazoendeshwa na mradi wa USAID Tuboreshe chakula.
Kikundi maarufu cha ngoma wilaya kongwa kata ya Ngomai kikitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa virutubishi  zinazoendeshwa na USAID Tuboreshe Chakula katika kata ya Ngomai wilayani Kongwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...