Meneja Mfuko wa LAPF, Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Amina Kassim, akizungumza na Waandishi wa habari, kuwapongeza waalimu wapya, jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Umewapongeza walimu wote kwa kupata ajira huku ikiwakumbusha kuwa huu ndio mwanzo wa maisha yao ya  ajira hivyo ni muhimu kujipanga vizuri kimaisha kwa kuchagua mfuko wa pensheni wenye maslahi bora!.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Amina Kassim wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea maendeleo ya zoezi loa uandikishaji waalimu wapya!.

Bibi Kassim amesema, maisha si mazoezi kwamba utarekebisha kesho, fanya umaamuzi sahihi sasa, kwa kujiunga na mfuko wa pensheni wa LAPF unaotoa mafao bora yatakayowawezesha kuyapatia maisha toka mwanzo kwa mafao bora katika mfumo ambao mwajiri anakuchangia.

Bibi Kassim amesema, Mfuko wa Pensheni wa LAPF, umeelezea mwamko mkubwa kwa waalimu wapya kujiunga na mfuko huo, na  kuwahimizi walimu wapya waliobakia kufanya uamuzi wa busara, kwa kujiunga na mfuko utakaowapatia maslahi bora.

Bibi Kassim amesema zoezi linakwenda vizuri, ambapo mfuko huo umefanikiwa kuwasajili waalimu wengi, kivutio kikubwa kinachowafanya waalimu wengi kuuchagua mfuko wa LAPF, ni licha ya mfuko huo kutoa mafao bora kabisa, mfuko huo wa LAPF pia unatoa fao la Uzazi, ambapo wengi wa waalimu wapya, kwa sababu ndio kwanza wanaanza kazi, huo pia ndio mwanzo wa ujenzi wa familia, hivyo fao hili kuonekana kuwa ni kivutio kikubwa kwao.

Bibi Kasim aliwasisitiza waalimu wapya ambao bado hawajakata shauri ni mfuko gani wa kujiunga, kuepuka kufanya maamuzi kwa kufuata mkumbo, bali kwanza wajiridhishe na ubora wa mafao yanayotolewa na mfuko husika ndipo waamue kujiunga kwa sababu ni haki yao ya msingi kabisa, kupata kilicho bora.

Mafao yanayotolewa na Mfuko wa LAPF ni pamoja na, Mafao ya Uzeeni (Old age), Mafao ya Mirathi (Survivors), Mafao ya Ulemavu (Invalidity), Mafao ya Uzazi (Maternity), Msaada wa Mazishi (Funeral Grant), Mafao ya kujitoa kazini (Withdrawal). Mafao ya Elimu, Mikopo ya Nyumba na Mikopo ya SACCOS

Zoezi la uandikishaji wanachama wapya wa mifuko ya hifadhi za jamii, ni zoezi linaloendelea kwa kipindi chote cha uhai wa mifuko, ila huwa linapamba moto zaidi wakati kunapotea ajira mpya kwa wingi kwa wakati mmoja, kama sasa ambapo serikali imetoa ajira mpya kwa waalimu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...