Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,atembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ya Maji,Makaazi na Nishati Nd,Ali Halil Mirza,(wa pili kushoto) wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja.
Uwanja wa mapembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika matengenezo,ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara leo ya kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh,(kushoto) wakati alipotoa maelezo ya ramani ya kiwanja cha Mapembea Kariakoo Mjini Unguja,alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh,(kushoto) kuhusu ujenzi wa kiwanja cha Mapembea Kariakoo Mjini Unguja,alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali maalim Abdalla Mzee wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo,(kulia) Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,na (kushoto) Katibu Mkuu Bi Mwanaidi Saleh.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...