Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa Simba waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kadi za akaunti za benki hiyo kwa ajili ya wanachama na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga leo katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa akimkabidhi mtangazaji Ephraim Kibonde wa Clouds FM mfano wa kadi ya akaunti ya benki hiyo hafla ya uzinduzi wa kadi za akaunti za benki hiyo kwa ajili ya wanachama na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga leo katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni msemaji wa Simba Bi Asha Muhaji na kulia ni Afisa habari wa wekundu hao wa Msimbazi Bw. Kamwaga
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa akimkabidhi mmoja wa mashabiki wa Yanga kadi ya akaunti ya benki hiyo hafla ya uzinduzi wa kadi za akaunti za benki hiyo kwa ajili ya wanachama na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga leo katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni msemaji wa Simba Bi Asha Muhaji na kulia ni Afisa habari wa wekundu hao wa Msimbazi Bw. Kamwaga
Kadi ya akaunti ya Benki ya Posta kwa mwanachama wa Yanga, ambapo wao wameanza na wanachama kufungua akaunti na kupata kadi hii, na baada ya miezi mitatu mashabiki watafanya hivyo
Kadi ya akaunti ya Benki ya Posta kwa mwanachama wa Simba. Tofauti na Yanga kadi za Simba zitaanza kugawiwa kwa mashabiki ambao watafungua akaunti, na baada ya miezi mitatu wanachama watapata fursa hiyo. Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii.
Je ni Vipi Kadi za Benki kwa Mabingwa Wapya wa Soka la Tanzania AZZAM ?
ReplyDeleteHahahahahah!
ReplyDeleteBenki ya Posta wabunifu sana, wameelewa ktk Simba na Yanga ndipo pa kuwashika watu kirahisi.
Mimi nitakata Rufaa Mahakamani kuweka pingamizi.
ReplyDeleteKwa kuwa hata hao Simba na Yanga wana Wababe wao ilibidi pia na Timu hizo za Vishoka wengine Mgambo JKT na JKT Ruvu pia wapewe Kadi za Benki, kama Mgambo JKT(Wababe wa Yanga) na JKT Ruvu(Wababe wa Simba)!