Familia ya Marehemu Mzee Augustine Cassian Mwingira kutoka Mjimwema, Kigamboni inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao, mzee Augustine Cassian Mwingira kilichotokea Jumanne, 27 Mei 2014 ktk Hospital ya Hindu Mandal alipolazwa baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Msiba upo Nyumbani kwa Marehemu Mjimwema, Kigamboni "Kwa Mwingira".
Ratiba ya Mazishi ni kama ifuatavyo;
Ijumaa, 30 Mei 2014
Saa 10 Jioni - Mwili wa Marehemu kuwasili Nyumbani kwake Maweni - Mjimwema, Kigamboni.
saa 11 jioni - Misa/Ibada ya kumuombea marehemu itakayofanyika hapo hapo nyumbani
Saa 1 usiku - Chakula cha jioni
Baada ya hapo ni sala na maombi mbalimbali yataendelea
Jumamosi, 31 Mei 2014
Saa 4 Asubuhi - Misa Takatifu
Saa 5 Asubuhi - Chakula
Saa 6 Mchana - Heshima za mwisho kwa Marehemu
Saa 7 Mchana - Safari ya kuelekea Makaburi ya Kinondoni
Saa 8 Mchana - Shughuli za Mazishi kwenye Makaburi ya Kinondoni (Ndani)
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe - Amen
Alikuwa mkuu wa mkoa wa wapi vile?
ReplyDeleteArusha.Pia wazi wa mawasilina na uchukuzi
ReplyDeleteMkoa wa Mara na Arusha.
ReplyDelete