Wakazi wa kijiji cha Kiwere wilayani Iringa
vijijini wametoa shukrani zao za dhati kwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la
Marekani (USAID) na kwa Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo
(LEAT) kwa kuendesha mradi wa ‘Ushiriki wa wananchi katika kusimamia maliasili’.
Akiongea wakati wa tathimini ya mafunzo ya mradi,
kiongozi wa kikundi cha kuhifadhi mazingira (Kiwere Hifadhi Mazingira), Hamza
Chang’a alisema, kabla ya mradi alikuwa na uelewa wa kawaida kuwa ukataji miti
hauruhusiwi kwa kuwa unaharibu mazingira, hakuelewa kuwa wananchi wanao wajibu
wa kulinda mazingira na maliasili kwa maendeleo endelevu na kuwa jambo hilo
limeelezwa katika katiba ya nchi.
“Nilipoona watu wakikata miti, niliona ni jambo la
kawaida, sikufahamu athari ya muda mrefu itokanayo na vitendo hivyo, namna vianavyo
athiri ubora wa maisha ya sasa na vizazi vijavyo.
"Nilidhani ni wajibu wa kamati
ya maliasili ya kijiji na viongozi wa kijiji kulinda maliasili, aliongeza.
Alisema mafunzo yamemwongeza ufahamu,
yamebadilisha mtazamo kuhusu usimamizi wa maliasili, na ameanza kutumia ujuzi
wake kwa vitendo kama mwananchi muwajibikaji.
Aliendelea kusema kuwa amepata dhana kamili ya
ushiriki katika michakato wa maendeleo hivyo atajitolea kushawishi, kufanya
kampeni na kufuatilia utekelezaji wa huduma za jamii.
Baada ya mafunzo, Chang’a na wenzake 16 waliunda
kikundi cha kuhifadhi mazingira na katika kipindi cha miezi minne wamepanda
zaidi ya miti 45,000 aina ya Mijoholo na Mikaratusi. Miti hiyo itapandwa katika
eneo la msitu wa Msuni lilio haribiwa kutokana na ukataji miti hovyo na
uchomaji mkaa.
Kwa upande wake Devotha Mihayo alisema, amejifunza
kuwa uharibifu wa mazingira una athari kubwa kwa jamii hususan kwa wanawake.
Unaathiri vyanzo vya maji, unasababisha ukame na njaa katika jamii. ‘Iwapo
vyanzo vya maji vita haribiwa tutalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji,
ambapo utatupotezea muda na kuweka maisha na afya zetu hatarini’ alisisitiza.

Kiongozi
wa ‘Kiwere Hifadhi Mazingira’, Hamza Chang’a na mwanakikundi Bruno Mpagama wakionesha
sehemu ya miti 45,000, waliyootesha katika bustani kijijini Kiwere


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...