Karandinga la Polisi likiwashusha Raia hao wa Ephiopia walioingia nchini kinyemela

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa  Iringa imewahukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh Milioni 1.5 kila mmoja, dereva Hansi Mwakyoma (28) na utingo wake wake Alex Adam (32) baada ya kukamatwa na kukiri kusafirisha wahamiaji wasio na vibali 83 kutoka nchini Ethiopia ambao pia wamehukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya Sh Milioni 1
Kwa kutumia gari aina ya Scania lenye namba T478 DFE mali ya Frola Mwambenja wa Mbeya, Januari 16, mwaka huu; dereva huyo na tingo wake walikamatwa katika kijiji cha Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo mkoani Iringa, barabara kuu ya Iringa Mbeya wakiwasafirisha watu hao kuelekea Kyela ambako ni mpakani mwa Tanzania na Malawi.
Akitoa hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa Endrew Scout alisema ameridhika na maelezo yaliyotolea na wakili wa serikali pamoja na vielelezo likiwamo gari lililotumiwa na watuhumiwa hao kusafirisha watu hao kutoka Kongowe Dar es Salaam kuelekea Kyela Mbeya.
Baada ya kusoma hukumu hiyo, baadhi ya raia hao wa Ethiopia waliangua kilio mahakamani hapo na kusababisha watu waliokuwa karibu na jengo hilo kusogea ili kujionea kulikoni.
Mkalimani wa wahamiaji hao ambao hawazungumzi Kingereza wala Kiswahili zaidi ya lugha ya kwao, Emanuel Yeb Mtaltisili  ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio ya Ebony FM cha mjini Iringa alisema; “walichokitarajia wahamiaji hao ni kupewa hukumu ya kurudishwa kwao baada ya kukiri kosa hilo.”
Awali akisoma maelezo ya kosa la watuhumiwa hao baada ya watuhumiw a wote kukiri kosa mbele ya mahakama hiyo, Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji Godfrey Ngwijo alisema ilikuwa Januri 16 mwaka huu katika eneo la Ruaha Mbuyuni watuhumiwa hao walipokamatwa wakiwa ndani ya gari hilo lenye bodi lililofunikwa wakisafiri kutoka Kongowe Jijini Dar es Salam kwenda Malawi kinyume na sheria ya uhamiaji ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015.
Alisema katika tarehe isiyojulikana, watuhumiwa 83 raia wa Ephiopia waliingia nchini kwa kutumia kwa njia zisizo halali na kuelekea jijini Dar es Salaam walikoanzia safari yao ya kuelekea Kyela mkoani Mbeya ili waingie nchini Malawi.
Alisema walipofika eneo la Ruaha Mbuyuni walikamatwa na Askari wa kikosi cha Usalama barabarani ambaye aliwataka wafungue mlango wa nyuma ya gari na kukuta kuna watu hao huku baadhi yao wakiwa hoi.

Alidai mara baadaya kukuta watu aliwaamuru kwenda kutuo cha Polisi cha Ruaha Mbuyuni ambako dereva na msaidizi wake walikiri kosa wakidai walikubali kuwasafirisha kwa makubaliano ya kupata kiasi fulani cha fedha na kwamba walipoona mzigo mkubwa waliomba waongezwe na kukubaliana na mwenye mzigo kuwa wangeongezewa  mara baada ya kufika walikokuwa wanakwenda.
Mara baada ya maelezo hayo ya wakili hakimu aliwataka watuhumiwa wote pamoja na kukiri kosa kuhojiwa kama wanayakubali maelezo hayo ili haki iweze kutendeka na walipoulizwa wakikiri kuwa maelezo yote yaliyotolewa na wakili wa serikali ni ya kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. KUWAFUNGA NI HASARA KWETU BOLA WANGEWARUDISHA KWAO

    ReplyDelete
  2. Put them on plane ndege yao si inakuja kila siku kwanini mnaingia gharama isiyo ya lazima

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa warudisheni kwao kufungwa ni kuongeza garama kwenye jela zetu ambazo hazitutoshi

    ReplyDelete
  4. si tunaimba kila siku kuwa Afrika ni moja. umoja gani huu!????

    ReplyDelete
  5. Hasara tu hio ya kuwafunga miaka yote hio...deportation ndo mpango mzima hamuoni kwa wenzenu???

    ReplyDelete
  6. Bora wangewafunga miezi 2 alafu kwao. Lkn hivi ni hasara kubwa kwa taifa

    ReplyDelete
  7. MBONA TANZANIA HAKUNA DEMOCRASY HAO SIO KRIMINALS HAO NI WAKIMBIZI AMBAO WANAKIMBIA KUTOKA KWAO KWENDA KUTAFUTA MAISHA MAZURI HAWAJAMUIBIA MTU WALA KUMPIGA MTU WALA KUNYANGANYANYA PESA YA MTU ,WAO NDIO WAMEPOTEZA PESA SAO KWA AJILI YA MALIPO KUVUSHWA UPANDE MWINGINE HIO SIO HAKI YA BINADAMU KABISA , NA DUNUA NZIMA ITAPINGA HUKUMU HIO ACHENI WENDAWAZIMU TANZANIA LAZIMA UBINADAMU UWEPO. INA MAANA WAKIMBIZI WOTE WALIOTOKA KWA SADDAM HUSSEIN NA HAWA WAPYA WANAOKIMBILIA ULAYA KUTOKA SYRIA VILE VILE WAFUNGWE JELA KAMA WAHALIFU? NO NO NO NI MAKOSA MAKUBWA YA JUDICCIARY YA TANZANIA,. STOP THAT, NOW WANAHITAJI MSAADA HAO SIO KUFUNGWA JELA KAMA WEZI, INA MAANA HATA MSAADA WA MWANASHERIA HAWAKUPATA ,ACHENI HIVYO TANZANIA

    NI MIMI MDAU UK,HUKU TUNAPINGA KABISA HUKUMU HIO HASA KWA WAAFRIKA WENZETU . SHAME ON US TANZANIANS

    ReplyDelete
  8. Warudisheni kwao tu. Tunaingia hasara kuwafunga. Kuwafunga ndio kitu gani tena hicho?? hawa ni wanyonge Fulani tu ambao walikuwa wanatafuta riziki tu. Ni shida tu ndo inayowazungusha kote huko. Sasa jamani busara nayo itumikage kwa hawa waafrika wenzetu.

    ReplyDelete
  9. Kwa nini msiwarudishe kwao?
    Mnawafunga kwa gharama zetu wenyewe.

    ReplyDelete
  10. Garama za kuwarudisha kwao watu 83 ni kubwa kuliko kuwafunga,cha maana hapa ni kuwaomba ubalozi wa Ethiopia wachukue raia wao wawasaidie kuwarudisha kwao.

    ReplyDelete
  11. Hao raia wenyewe watafurahi........Na hapo ni kuliongezea gereza gharama zisizostahili wakati fedha hizo za kuwagharamikia zaweza fanya vitu vingine vya kuwaboreshea mazingira....Wangerudishwa kwaoo...

    ReplyDelete
  12. Hawa warudishwe kwao tu, kuwafunga watatulia kodi zetu tu. Hata hio kuendesha kesi imetupotezea fedha, hawa ilikuwa kurudishwa kwao immediately, bora hasara ya kuwasafirisha.

    ReplyDelete
  13. SHAME ON TANZANIA

    ATI MNABANAMATUMIZI

    ReplyDelete
  14. Ethiopia airways ipo tumbukiza waende

    ReplyDelete
  15. Sasa hapa waafrika ndipo tunapochekwa na wazungu. Wenyewe kwa wenyewe tunafanyiana ukatili. Toka lini mkimbizi akatiwa jela. Mngewakuta wazungu kigrupu kama hicho na kesi kama hiyo hiyo mngewafunga kweli??kwahiyo kule Afrika kusini na nchi zingine watanzania wasio na vibali nao ni sawa wakifungwa??hii nayo sasa kali. embu wapakizeni ndege yao waende kujitafutia maisha kwingine khaa!kuweni na huruma na waafrika wenzenu jamani. mkimbizi hafungwi ila anasaidiwa au anarudishwa kwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...