Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili katika kata ya Hembeti, Kijiji cha Dihinda kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima nawafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.

Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.


Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi siku hizi raia wanaruhusiwa kuvaa mavazi ya kijeshi kama alivyofanya waziri nchemba?

    ReplyDelete
  2. Kuua mifugo ya mjane mmemusa Muumba wake mboni ya jicho. Chavuyemo

    ReplyDelete
  3. Sub'hanallah! Kweli inatilisha imani, pole sana Mama wa watu tena mjane, hata imani binaadam hatuna imetutoka kabisa! Pengine Mama huyo mjane alikuwa anajipatia rizki yake ya halali kupitia humo humo kwenye mifugo yake, leo hii mmekwenda kumcharangia kwa mapanga mifugo yake tena mizima mizima na kuiteketeza yote, analia maskini kwa uchungu na kufikiria mengi. Pole Mama mjane wa watu, Mwenyeez Mungu anashuhudia yote hayo na In Sha Allah atakulipia pia kukujaalia wepesi katika kutarazaki kwako licha ya kuwa wamekuangamizia kipato (mifugo yako). Tufike wakati jamani tukumbuke dunia ni ya kupita tu, tuuthamini utu tusitokwe imani kwa ajili ya vitu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...