Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam
(Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji kwenye operesheni yake maalumu ya
kubaini watumiaji wa huduma ya Maji ambao hawajaunganishiwa kihalali kwenye
mtaa wa Ilala kota karibu na nyumba za Shirika la nyumba la taifa (Nhc) jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye tukio hilo Meneja wa Dawasco Ilala,
mhandisi Ramadhani Mtindasi alieleza kuwa wanatekeleza agizo la Mh. Waziri wa
Maji ambapo amewaagiza Dawasco kufunya uchunguzi kwenye Magorofa yote makubwa
jijini ambayo wanadai wanatumia Maji ya visima na ndipo walipogundua jengo hilo
la ghorofa lenye nyumba ndogo (apartments) 8 likiwa na laini mbili moja ya Maji
ya kisima na nyingine ni ya Dawasco ambayo haikuwa na mita wala kusajiliwa na
Dawasco .
“Tumeanza operesheni maalum ya kukagua majengo
yote makubwa jijini ambayo wanatumia huduma ya Maji ilikubaini kama ni ya
visima au ya Dawasco kama Mh. Waziri wa Maji alivyotuagiza na ndipo tulipogundua
jengo moja eneo la Ilala kota likiwa na laini ya Maji ya Dawasco ila halina
mita wala hatujamsajili amejiunganishia kiholela”
“Hivyo tuwewashirikisha serikali za mitaa kubaini
mmiliki wa jengo hilo lakini hakuweza kufahamika bali tumepata namba zake za simu
na tulipompigia alidai anatumia huduma ya Maji ya kisima tu hivyo tumemuandikia
barua afike kwenye ofisi zetu kujisali na alipe faini”, alisema mhandisi
Mtindasi.
Kwa upande wa mjumbe mtaa wa Ilala Kota Bi Habiba
Hamisi ameeleza kuwa Majengo mengi makubwa yamekuwa yakijiunganishia huduma ya
Maji kiholela na kudai kuwa ni ya kisima kumbe sio hivyo kuwafanya wananchi
wengine waotegemea huduma ya Maji ya Dawasco kukosa kutokana na kuwa majengo
hayo makubwa yana matumizi makubwa.
“Majengo mengi makubwa yana laini mbili ya Dawasco
na visima ila ukiwauliza wasema wanatumia maji ya visima tu kumbe sio kweli na
matumizi yao kwenye majengo hayo ni makubwa hivyo wanasabisha wanaostahili
kukosa huduma ya maji hivyo Dawasco wawachukulie hatua kali za kisheria” alisema
Bi Hamisi.
Dawasco imewasihii wamiliki wote wa majengo
makubwa ambao wamejiunganishia huduma ya Maji Kiholela kujisalimisha mapema
kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa juu yao endapo watakamatwa.
Meneja wa Dawasco llala (katikati) Mhandisi Ramadhani Mtindasi pamoja na mjumbe wa mtaa wa Kota Bi. Habiba Hamisi akionyesha bomba la Maji ambalo linaleta Maji kutoka kwenye laini kuu lilo uunganishwa kiholela inayotoka kwenye Bomba kubwa kwenye eneo la Ilala Kota Mchikichini Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Dawasco Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi akionyesha boza linalotumika kuhifadhi Maji yanayotoka kwenye bomba la Dawasco .




sababu moja ya watu kuiba maji ni kwa sababu idara ya maji wanataka kuhongwa ili waunganishe maji. Mteja anapokuwa amelipia gharama zote za maji na amenunuwa vifaa ili idara ya maji waje kuunganisha maji huwa ni kiama. Kwa hiyo Idara ya maji wasijifanye kuwa hawahusiki na hii hali, wao ndiyo CHANZO KIKUBWA CHA WIZI HUU. Wakuu fanyeni utafiti mutabaini hivyo.
ReplyDeleteWewe mhandisi wa dawasco kwanza acha propoganda ya kuonyesha kwamba unafanya kazi kwa mkurugenzi wako ofisi yako safisha ofisi yako kwanza mbona ofisi yako inaongoza kwenda kujirusha eti mumefuka malengo....... wakati mna babikiza madeni sio halali????????????
ReplyDelete