Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford, maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo pichani) ramani ya Mkoa wa Dar es salaam aliyoitumia kutambua maeneo ya Mkoa huo.

 Hiyo ilikuwa baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais John Pombe Magufuli ili kumpongeza kwa kuwajumuisha wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la Mawaziri. Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kutimiza adhma yake hiyo.
Msanii Joseph Starnford maarufu kwa jina la Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Baraza lake la Mawaziri, amesisitiza kuwa shauku yake ni kuonana na rais ili kutimiza adhma yake.
Zaidi Bonyeza HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbona hiyo ramani aliyoshika ni ya Tanzania na siyo Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  2. Hawajamtendea haki huyu kijana mzalendo kwa kutompa nafasi ya kusema hata hello kwa Rais baada ya kujitolea namna hii. Sijapenda kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...