IKIWA ni siku chache tangu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuwasihi wenyeviti wa serikali za mtaa kubani wezi wa Maji kwenye maeneo yao,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) kupitia operesheni yake maaalum ya kukagua majengo makubwa kwenye maeneo ya jiji, limebaini wizi mkubwa wa Maji nyumbani kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Amana Ilala jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwenye tukio hilo Meneja wa Dawasco Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema kuwa wamebaini wizi huo wa Maji kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambaye ameweza kufahamika kwa jina moja la bi Zainabu baada ya kufanya uchunguzi ambapo laini za Maji zimeunganishwa moja kwa moja kwenye visima viwili vilivyopo kwenye nyumba hiyo nakudai kuwa mara zote wenye nyumba hao wamekuwa wakidai Maji wanayotumia niya kisima mpaka walipofanya uchunguzi nakugundua wizi huo.
“Tumeweza kugundua wizi wa Maji nyumbani kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambapo tumeweza kupata jina lake moja la bi Zainabu kwa kuwa alikimbia tulipofika kwenye eneo la tukio ila tulifanya uchunguzi kwenye nyumba yake na kubaini kuwa ameunganisha laini za Maji moja kwa moja kwenye visima vyake viwili vilivyopo nyumbani kwake na mara zote huwa anadai anatumia Maji ya Kisima kumbe anafanya wizi wa Maji”,alisema Mtindasi.
Hata hivyo meneja wa huyo amesema kuwa walifanyiwa fujo na vijana wa nyumba hiyo walipofika kufanya uchunguzi na kusababisha moja wa mafundi wa Dawasco kujeruhiwa, kutokana na tukio hilo la kushambuliwa wamechukua hatua za kuripoti polisi nakuandikisha hati ya kukamatwa (RB)kwa vijana hao pia wameng’oa mabomba yanayopeleka Maji kwenye visima vilivyopo kwenye nyumba hiyo nakuwatoza faini ya Maji ya wizi waliyokuwa wakitumia.
“tulivyofika kwenye eneo la tukio kwa ajili ya` kufanya uchunguzi tulifanyiwa fujo nakupelekea mmoja wa Mafundi wetu kujeruhiwa ila tumechukua hatua mbalimbali ikiwa naku ripoti polisi nakuandikisha hati ya kukamatwa kwa vijana hao pia kutokana na kugundua wizi huo pia tumeng’oa laini zote zinazopeleka Maji kwenye visima vya nyumba hiyo nakumtoza faini ambayo tutamuandikia barua ya kumtaarifu kiasi gani cha kulipa”, alisema Mtindasi.
Kwa upande wa majirani akiwemo bwana Hamisi Khaflan amesema kuwa atatoa ushirikiano kwa Dawasco ili kubaini vijana waliofanya fujo kwa mafundi waliokuja kuchunguza wizi wa Maji kwenye eneo hilo. “Tunahaidi Dawasco tutashirikiana nao kubaini vijana ambao wamewafanyia fujo kwa kuwa tunawafahamu na pia kitendo walichokifanya vijana hao sio kizuri na wamevunja sheria”,alisema Khalfan.
Hata hivyo mpaka taarifa inafika mtamboni mwenyekiti huyo alikuwa amekimbia, Dawasco inaendelea kuwasihi wakazi wote wa jiji la Dar es salaam waliojiunganishia kinyume na utaratibu kujisalimisha iliwaweze kuunganishiwa huduma ya Maji kihalali kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kwa wizi wa Maji.
Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) Ilala akionyesha moja ya kisima cha Maji ambacho kilichounganishiwa moja kwa moja laini ya Maji kinyume na utaratibu kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa mtaa eneo la Amana Ilala jijini Dar es salaam.


Wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa ni wala rushwa wakubwa. watumbuliwe tu
ReplyDelete