Na Mwandishi wetu.
SERIKALI imesema kuwa italipa kipaumbele suala la uhakiki wa mali za viongozi wa umma kwa kuiwezesha Sekretarieti ya Maadili ya viongozi kufanya kazi zake kwa ukamilifu kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma kujua majukumu, mafanikio na changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo ili wakifika bungeni waweze kuisemea.
“Suala la uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi tutahakikisha linapewa kipaumbele katika Awamu hii ya tano ya uongozi,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, Serikali itajitahidi kuongeza jitihada ili uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi wa Umma ufanyike, pamoja na kuiongezea Taasisi hiyo bajeti ya kutosha.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...