Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika moja ya kikao na wakandarasi wanaosambaza Umeme Vijijini vilivyoanza tarehe 29 Machi na kumalizika tarehe 31 mwezi huu.Wa Tatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi kutoka REA, Mhandisi Bengie Msofe. Wengine ni watendaji kutoka kampuni ya Angelique International inayosambaza umeme mkoani Arusha, Wizara na REA.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na kampuni ya Engineering & Construction inayosambaza umeme vijijini mkoani Kagera katika wilaya za Ngara, Biharamulo, Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Bukoba vijijini na Muleba kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya na anayemfuatia ni Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga.Wengine ni watendaji kutoka kampuni hiyo, Wizara na REA.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa kwanza kushoto), Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga (wa pili kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya (wa Tatu kushoto) wakiwa katika moja ya vikao vilivyojumuisha wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini vilivyoanza tarehe 29 Machi na kumalizika tarehe 31 Machi, mwaka huu.
Na Teresia Mhagama.
Imeelezwa kuwa wakandarasi wenye tuhuma za kutolipa mishahara wafanyakazi wao, kuomba rushwa kwa wateja wanaotaka kuunganishiwa umeme na kutolipa fedha za watoa huduma waliokuwa wakifanya nao kazi katika usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili, hawatapewa kazi husika katika miradi ya REA Awamu ya Tatu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na kampuni mbalimbali zinazotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili inayotarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...