Wakazi wa Kata ya Kibamba wamepiga kura ya siri kuwabaini
wahalifu wanaoishi katika maeneo yao kufuatia tukio la karibuni la uvamizi
katika nyumba nne zilizopo Mtaa wa Muhongoni ambalo limesababisha kifo cha
mkazi mmoja wa eneo hilo, aliyejulikana kwa jina la Julius Msalangi.
Upigaji kura huo ulifanyika katika mkutano wa hadhara
ulioitishwa na ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ambao ulifanyika
viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata na kuhudhuriwa na Kamanda wa Polisi wa
Kata ya Kibamba, Pius Lutumo.
Uamuzi wa kupiga kura hiyo umetokana na kuanza kuibuka kwa
vitendo vya ujambazi unaofanywa majumbani na makundi ya vijana, uporaji wakati
wa alfajiri na wizi wa mifugo hali ambayo imesababisha watu kadhaa kujeruhiwa
na wengine kupoteza mali zao.
Katika mkutano huo, wakazi hao walikubaliana na kupiga kura
za siri ambazo ziliwataja mara nyingi watuhumiwa wa uhalifu sugu wanne ambao
Diwani wa Kata hiyo, alisema hata yeye majina yao ameyakuta ofisini kwake hivi
karibuni alipoingia madarakani hivi karibuni.
Diwani wa kata hiyo, Ernest Mgawe aliwataka wakazi wa kata
hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na ofisi yake hasa pale yanapotokea
matukio ya uhalifu nna kukamatwa kwa watuhumiwa ili lengo la kuifanya Kibamba
kuwa sehemu salama ya kuishi liweze kufikiwa.
”Tunaomba ushirikiano wenu kwani kuna wakati watu walivamiwa
na kujeruhiwa na mmoja kati ya watuhumiwa sugu ambaye pia leo ametajwa lakini
hata hivyo wahanga walipotakiwa kwenda olisi kutoa maelezo ili mlenga afikishwe
maakamanbi hawakuonekana” alisema.
Awali Kamanda wa polisi wilaya ya kipolisi ya Kibamba
aliwataka wananchi watambue kuwa suala la ulinzi na usalama ipo miononi mwao
kutokana na hali halisi ilivyo hvi sasa na kuwataka waachane na nadhjaria kuwa
polisi ndi walinzi wao na mali zao.
“Hilo mnapaswa kjulitambua na kulingana na sheria ndogo
zilizotungwa katika manuspaa ya ionondoni suala la ulinzi shrikishi sio iyari
hasa pa,e wananchi wanapokubaliana upitia mikutano yao halali kma huo” alisema.
Alibainisha kuwa kura za siri zilizopigwa zitafanyiwakazi na
kila mkazi ni lazima ashiriki ulinzi huo iwe kwa yeye mwenyewe kutoka na
kulinda au kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya uwezeshaji wa mpango huo na wale
ambao watakaidi watafikishwa mahakamani kwani sheria ipo wazi.
Pia Diwani Mgawe amewapa siku 30 watu wanaomiliki maeneo
katka kata hiyo ambayo hawajayaendeleza hivyo kuwa mapori ambayo sasa
yanatumiwa kama maficho ya wahalifu na baada ya muda hup atawasilisha majina
kwa mkuu wa mkoa kwa aili ya hatua zaidi.
Alisema kuna maeneo mengi eneo hilo ambayo wamiliki wake
hawayaendelezi na yamegeuka mapori na ingawa wengine wana hati za kuyamiliki
lakini wataomba msaada ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi ili kuwanusuru wananchi na
madhila ambayo wanayapata hivi sasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...