Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya
mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo ili iweze kujadiliwa na
wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Katika ripoti yake, CAG
ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha
matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo yanayokusudiwa.
Miongoni mwa maeneo
ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa nchini
ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa wakati kulingana na
matakwa ya sheria.
Hatua hiyo ya CAG
inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu
ambavyo jumla yao ni vyama 22.
Prof. Assad alisema kuwa
kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja ndicho
kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi
Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).
Vyama vingine 21
havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha kifungu Na.
14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya
mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya
mwaka 2016/2017.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha
unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti
ya mwaka 2016/2017.
Waandishi wa habari
wakipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze
kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...