Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (katikati) akikata utepe kuzindua Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Vito Arusha (AGF), Peter Pereira, Wa Pili Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA), Sammy Mollel na wa Pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (wa kwanza kulia) akiwa katika banda la mdanyabiashara wa madini ya Vito, Bhadrash Pandit katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016. Kulia kwa Mkuu wa wilaya ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila (kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (kulia) wakiwa katika kikao na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Vito ya Arusha yanayofanyika katika hoteli ya Mount Meru.
Baadhi ya madini ya Vito yanayopatikana katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016 katika Hoteli ya Mount Meru.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akifungua maonesho ya kimataifa ya madini ya Arusha Gem Fair kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda leo katika hoteli ya Mount Meru . 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sioni maana ya maonyesho hayo. Tukumbuke kuwa Rais alisema kuwa, "madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania lakini nchi zinazoongoza kwa kuuza ni india na Kenya". hii ina maana hawa viongozi wetu kwenye nyanja hii hawajui walifanyalo,hivyo hakuna maana yoyote ya haya maeonyesho. Tubalike tuwe na moyo wa kujituma na tuwe wadadisi,tusijibweteke tu kutegemea wageni watusaidie.
    Ni maoni yangu tu...

    ReplyDelete
  2. maonesho kama haya yamekuwa ni njia ya kutangaza madini ya tanzanite kutoka Tanzania na kuhamasisha wageni kutoka nje kununua madini ya tanzanite yenye cheti chenye kuonyesha uhalisia wa nchi yanakotoka ambayo ni Tanzania. Tusibeze kila kitu kinachofanywa na serikali, juhudi za kudhibiti utoroshaji zinafanyika na serikali na maonesho hayo yamekuwa ni sehemu kupiga mnada madini yanayokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...