Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (katikati) akikata utepe kuzindua Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Vito Arusha (AGF), Peter Pereira, Wa Pili Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA), Sammy Mollel na wa Pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (wa kwanza kulia) akiwa katika banda la mdanyabiashara wa madini ya Vito, Bhadrash Pandit katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016. Kulia kwa Mkuu wa wilaya ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila (kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (kulia) wakiwa katika kikao na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Vito ya Arusha yanayofanyika katika hoteli ya Mount Meru.
Baadhi ya madini ya Vito yanayopatikana katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016 katika Hoteli ya Mount Meru.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akifungua maonesho ya kimataifa
ya madini ya Arusha Gem Fair kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix
Ntibenda leo katika hoteli ya Mount Meru .
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (wa kwanza kulia) akiwa katika banda la mdanyabiashara wa madini ya Vito, Bhadrash Pandit katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016. Kulia kwa Mkuu wa wilaya ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila (kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu (kulia) wakiwa katika kikao na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Vito ya Arusha yanayofanyika katika hoteli ya Mount Meru.
Baadhi ya madini ya Vito yanayopatikana katika Maonesho ya Tano ya Vito- Arusha yaliyoanza jijini Arusha tarehe 19 na kumalizika Aprili 21, 2016 katika Hoteli ya Mount Meru.

Sioni maana ya maonyesho hayo. Tukumbuke kuwa Rais alisema kuwa, "madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania lakini nchi zinazoongoza kwa kuuza ni india na Kenya". hii ina maana hawa viongozi wetu kwenye nyanja hii hawajui walifanyalo,hivyo hakuna maana yoyote ya haya maeonyesho. Tubalike tuwe na moyo wa kujituma na tuwe wadadisi,tusijibweteke tu kutegemea wageni watusaidie.
ReplyDeleteNi maoni yangu tu...
maonesho kama haya yamekuwa ni njia ya kutangaza madini ya tanzanite kutoka Tanzania na kuhamasisha wageni kutoka nje kununua madini ya tanzanite yenye cheti chenye kuonyesha uhalisia wa nchi yanakotoka ambayo ni Tanzania. Tusibeze kila kitu kinachofanywa na serikali, juhudi za kudhibiti utoroshaji zinafanyika na serikali na maonesho hayo yamekuwa ni sehemu kupiga mnada madini yanayokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi.
ReplyDelete