TAARIFA KWA UMMA
Mnamo tarehe 01.04.2016
ilisambazwa taarifa ya uongo kwenye mitandao ya Kijamii ambayo kwa kiasi
kikubwa ilipotosha Umma wa Watanzania kwamba
kuna Kikao cha Baraza la Madiwani
kilichokua kifanyike Tarehe 01.04.2016 kimevunjika na kuahirishwa hadi wiki
ijayo kufuatia Waheshimiwa Madiwani kutoa hoja ya kutojadiliwa kwa Kabrasha
mpaka hapo hoja mbili za nyuma zitakapojibiwa.
Tungependa wananchi
waelewe kwamba taarifa hiyo si sahihi na inapotosha umma. Halmashauri ya Jiji
la Arusha kama ilivyo Mamlaka zingine za Serikali za Mitaa Nchini inaendeshwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za uendeshaji
wa shughuli za Serikali za Mitaa na Taratibu za uendeshaji wa vikao vya
Halmashauri. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Halmashauti ya Jiji la Arusha kikao
cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilifanyika Feb 10, 2016 na kitaketi tena
baada ya miezi mitatu.
Hii ina maana kwamba
hakuna Kikao chochote kilichokua kifanyike Tarehe 01.04.2016 na wala hoja zilizotajwa
kwenye taarifa hiyo si za kweli. Vikao vyote vya Baraza la Madiwani hutangazwa
na Mkurugenzi wa Jiji kupitia vyombo vya Habari na viko wazi kwa Umma na
mwananchi yoyote anaruhusiwa kuhudhuria.
Inawezeakana mtoa
taarifa hizo pengine alikusudia kutumia tarehe 01 April kuwa siku ya wajinga
lakini hakupaswa kutoa uongo kwa Umma katika maswala ambayo upotoshaji wake
utaathiri jamii.
Napenda kuwaarifu
watanzania wote kuipuuzia habari hiyo kwani haina ukweli wowote.
IMETOLEWA
NA:
AFISA HABARI
Kny: MKURUGENZI WA JIJI
ARUSHA
02.04.2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...