Pichani chini ni baadhi ya wananchi wakiweka masalia ya Kichwa cha Mtoto, Nasra Mkinze
mwanafunzi wa Darasa la Pili, ambapo haikufahamika mara moja jina la
shule hiyo, baada ya kugongwa na Gari la Mwendokasi T 953 DGV kwa kile
kinacho daiwa chanzo ni Mwendesha Bodaboda MC 351 AWX kutaka kuwahi
mataa ya Shekilango Dar es Salaam mchana huu na ndipo Dereva huyo wa
mwendokasi kuruhusiwa na kumgonga akiwa amembeba Shemeji yake na mtoto
(akimwita baba mdogo) dereva wa Bodaboda walipokua wakienda mkoani Morogoro kwenye
arobaini . (PICHA NA KHAMISI MUSSA )
Msamaria Mwema akiweka ndani ya Gari la Polisi mwili wa mtoto Nasra Mkinze
mwanafunzi wa Darasa la Pili,
Wananchi wakiwa wamelizingira Gari la Mwendokasi.
Askari wa Usalama Barabarani akizungumza na wananchi eneo la tukio na Pikipiki iliyosababisha ajali hiyo ikiwa imezungukwa


Poleni wafiwa, kama ni alama za punguza mwendo au bumps kwenye maeneo ya vituo zinatakiwa maboresho yafanywe ili mwendo wa kasi usihatarishe maisha ya wengine..
ReplyDeletePoleni na msiba.
ReplyDeleteIla jamani kwani hakuna gari maalum za polisi kubeba maiti ? maana naona hii gari kama ya mizigo vile na ipo chafu.
So very sad, RIP little angel.
ReplyDeleteikiwa taa inamruhusu dereva kupita na chombo chake haimaniishi kuwa asiwe mwangalifu na wenye kwenda kwa miguu au wenye vyombo vingine , ni wajibu wake kuhakikisha kuwa ni salama kabla kuondoa chombo chake. Mara nyingi tumeona ajali zikisababishwa na dereva kwa kuwa tu eti taa inamruhusu basi yeye hajali chochote hata kama kuna mtu au chombo mbele yeye hugonga tu kwa kutarajia sheria itamlinda kwa kuwa alipita wakati taa inamruhusu
ReplyDeleteMagari ya mwendo kasi yana barabara yake maalum kwa hiyo ukigongwa nalo inamaanisha wewe ndio umeingilia barabara yake ambayo imetengwa kwa ajili ya yale ma basi tu na sio chombo kingine chochote kile.
ReplyDelete