Na Bashir
Yakub.
Katika saa za
kazi zipo saa
za kazi katika
siku za kawaida, saa
za kazi za ziada
na saa za
kazi katika siku
ambazo ni za
sikukuu. Kuna umuhimu mkubwa
sana kwa mfanyakazi kujua
masaa ya kazi .
Kama hujui masaa
ya kazi ya
kisheria basi ni vigumu
kujua usahihi wa
ujira unaolipwa .
Malipo ya
kazi hayatokani na
mshahara pekee. Yapo malipo
mengine ya ziada
yatokanayo na muda
wa ziada zikiwemo siku
za sikukuu. Ili ujue
usahihi wa kile
unacholipwa yakupasa kujua pia
mchanganuo wa masaa ya
kazi. Masaa ya
kazi yapo aina
mbili.
Yapo masaa
ya kazi ya
kawaida na yapo
masaa ya kazi
ya ziada. Sikukuu nazo
hujumuishwa katika masaa
ya kazi ya
ziada.
1.JE SAA
ZA KAZI NI NGAPI KATIKA SIKU ZA
KAWAIDA ?.
Katika siku za
kawaida saa za kazi
ni 9. Kwahiyo kwa siku
mfanyakazi anatakiwa kufanya
kazi masaa 9. Hii
ina maana atafanya
kazi masaa 45 kwa
wiki ikiwa atafanya kazi kuanzia
jumatatu mpaka ijumaa.
Muhimu sana katika
suala la saa za
kazi ni kuwa
mfanyakazi asifanye kazi zaidi
ya saa 45 kwa
wiki kwa masaa ya kawaida.Hata
siku zikizidi lakini
masaa 45 kwa wiki yasipite. Hayo ni
masaa ya kawaida.
2. JE
SIKU ZA KAZI
NI NGAPI ?.
Siku za kazi
zinazoruhusiwa ni sita
kwa wiki. Lakini itategemea na
taratibu za ofisi
yako. Zipo ofisi watakwambia tunafanya kazi jumatatu
mpaka ijumaaa na wapo wengine
watakwambia kazi ni
jumatatu mpaka jumamosi. Hawa wote
watakuwa hawajakosea kwasababu bado
wako ndani ya
ukomo wa siku
za kisheria.
Linalopaswa
kuzingatiwa hapa ni
kuwa vyovyote itakavyokuwa
masaa ya kazi
kwa wiki yasizidi
45. Iwe siku tano
kwa wiki au sita muhimu masaa
yasizidi 45 kwa
wiki. Haya ni
masaa ya kawaida.
Masaa ya kawaida
ni yale masaa ambayo
sio ya ziada.



Inakuwaje saa 9 za kazi kwa siku wakati tunafanya kazi saa 1.30 mpaka 9.30? Ukipiga mahesabu inakuwa saa 8 kwa siku. Na hii ni hata kwa wale wanaofanya kazi saa 2 mpaka 10.
ReplyDeleteJumla ya masaa kwa wiki yatakuwa ni 40 na siyo 45. Kwa kawaida jumamosi haimo isipokuwa kwa kazi maalumu za ziada, au nimekosea?