Na Tigaya Vincent_MAELEZO-Dodoma.

Wizara ya Afrika , Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha maabara nne za Kanda ili kuboresha huduma za vipimo vya upimaji wa kifuu na kifuaa kikuu sugu.Hatua hiyo inalenga kuimarisha na kusogeza huduma karibu za upimaji wa kifuaa kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha 2016/17.

Amezitaja hospitali hiso ambazo zitakuwa na maabara hizo kuwa ni Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Kibong’oto mkoani Kilimanjaro.Waziri Ummy aliongeza kuwa Wizara hiyo itaendelea matibabu ya kifua kikuu sugu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bugando.

Aidha ,Waziri huyo aliongeza kuwa Wizara imefanikiwa kufikia idadi ya vituo 547 vinavyotoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI nchini .Hatua hii inalenga kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wenye maambukizi mseto ya Kifuua Kikuu na UKIMWI kupata huduma sehemu moja.

Waziri Ummy aliongeza kuwa chini ya utaratibu huo , Wizara imefanikiwa kutoa huduma watu 692,642 wanaoishi na Virusi vinavyosababisha UKIMWI (WAVIU) ili kubainisha uwepo na kutokuwepo kwa maambukizi ya kifua kikuumiongoni mwao.

Alisema kuwa kati ya hao watu 26,218 waligundulika kuwa na maambukizi ya kifua kikuu na walipatiwa matibabu.Aidha , Waziri huyo alisema kuwa katika mwaka ujao wa fedha ,Wizara hiyo itaendelea kutoa huduma za matibabu ya kifua kikuu sugu kufikia hospitali kumi za mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Tanga, Shinyanga, Geita na Mara.

Alisema kuwa Wizara itaongeza uwezo mikoa 16 yenye viwango vya chini kabisa vya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ili kuongeza kasi ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.Katika mwaka ujao wa fedha Wizara hiyo iliomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya matumizi ya Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ys shilingi 845,112,920,056.00.

Kati ya fedha hizo shilingi 317,752,653,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...