Na Tiganya Vincent, Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa  iko tayari kutoa mafunzo maalum ya elimu ya fedha kwa wananchi wote wakiwemo wakinamama kuhusu ili kuleta uelewa mpana wa upatikanaji wa huduma za fedha na taratibu zinazohusu mikopo.

Kauli hiyo imetolewa leo mijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kachwamba Kajaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anna Lupembe aliyetaka kujua mipango ya Serikali ya kupeleka huduma za kibenki vijijini ili wanawake waweze kupata mikopo.

Aidha, alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imehakikisha kuwa huduma za kibenki zinawafikia wananchi wengi ili kurahisisha shughuli zao mbalimbali za kiuchumi katika maeneo ya mjini na vijiji.Alisema kuwa baadhi ya Benki zimeanzisha huduma za Kibenki kupitia mawakala, na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi ambazo zimewasaidia wananchi kwenye sehemu ambako hakuna matawi ya Benki.

Mhe. Dkt.Kajaji aliongeza kuwa  Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Benki Kuu inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kusaidia nguvu za wananchi na sekta binafsi kuanzisha benki au taasisi za fedha.

Alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kuzishawishi Benki kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo yao.Mhe. Dkt.Kajaji alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kushawishi Benki nchini kupanua shughuli zao ili ziwafikie wananchi wengi hasa wale wa vijijini wakiwemo akina mama.

Aidha, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na BOT iko tayari kutoa mafunzo maalum ya elimu ya fedha kwa wananchi wote wakiwemo wakinamama kuhusu utumiaji wa huduma za kifedha ili kuleta uelewa mpana wa upatikanaji wa huduma za fedha na mikopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...