Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam  pamoja na  Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 10 kuanzia saa 5 asubuhi Jumanne, Tarehe 17/05/2016.
Sababu za kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Chini ni kuzuia uvujaji uliotokea mtamboni kwenye bomba la inchi 72. Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es salaam kukosa Maji:
MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.
DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 
022-2194800 au 0800110064 (BURE)

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO-MAKAO MAKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2016

    TANGAZO HILI LIMECHELEWA KUTOKA LEO NI TAYARI TAREHE 17/05/2016 KWA HIYO HATUJANYA MAANDALIZI YOYOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...