Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam leo. wakati wa kufungua mafunzo ya maadili kwa wafanyakazi wa TRA ambao wamefanya usaili na kufanikiwa kufunzu kusoma mafunzo hayo kwa wafanyakazi kwaajili ya kujifunza mambo mtambuka ya tasinia ya TRA. Lengo la kuwapa mafunzo hayo ni kutaka kuijenga Mamlaka ya Mapato (TRA) mpya.Kulia ni Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasiliamali watu na utawala katika chuo cha Kodi(TRA), Victor Kimaro wakiwa katika mkutano wa kufungua mafunzo ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo akizungumza wakati wa hafla kufungua mafunzo ya awamu yapili ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Amesema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha Mungu katika kazi zao.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo wakikata utepe kuzindua ripoti ya mafunzo kwa wanafunzi wa malaka ya Mapato Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...