Na Lorietha Laurence-Maelezo
Baada ya kuanza rasmi kwa mabasi ya mwendo wa haraka Jijini Dar es
Salaam wananchi wameupokea kwa maoni tofauti huku wengi wao
wakisifia hatua hiyo ya serikali katika kurahisisha hali ya usafiri katika jiji
hilo.
Wakitoa maoni yao katika maeneo mbalimbali ya jiji ,Bw.Kulwa Khamis
Mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi mwisho amesema kuwa huduma hii ya
usafiri ni nzuri kwa kuwa haina foleni na inaokoa muda wa kusafiri.
“nimefurahishwa na huduma hii kwa kuwa haina foleni na inasaidia kufika
kwa wakati maeneo yetu ya kazi na hata kurudi nyumbani
mapema,jambo ambalo linapunguza muda mwingi uliokuwa ukipotea
katika foleni” alisema Bw.Khamis.
Naye Bi.Emmy Jonas mkazi wa Kibamba amesema kuwa huduma hiyo ni
nzuri lakini amedai kuwa nauli ni kubwa na kuomba uongozi wa Dar es
Salaam Rapid Transport (DART) na taasisi husika kufikiria upya nauli ili
wananchi wa hali ya chini waweze kumudu.
Aidha Bi. Jonas ameiomba serikali kumalizia miundombinu ya barabara ya
mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) ili yaweze kufika mpaka Kibaha,
badala ya Kimara mwisho ili kuepukana na usumbufu wa kupanda magari.
Kwa upande wake Mtaalam wa Mawasiliano wa BRT, Bw. Abraham
Nyatori ameiomba jamii ibadilike kuhusu utunzaji wa
miundombinu,“hakuna kitu kinaitwa mali ya umma”,amesisitiza Nyatori.
Mtaalam huyo alikuwa na maana kwamba kila mwananchi anatakiwa
kulinda na kuitunza miundombinu ili itumike kwa muda mrefu na kuiona
kama mali yake na siyo ya umma.
Serikali imekuwa ikijenga barabara katika maeneo mbalimbali jijini na
baadhi ya barabara hizo kuharibika baada ya muda mfupi na hivyo
kuigharimu serikali mamilioni ya fedha kwa ajili ya matengenezo badala
ya kujenga barabara zingine .



Mabasi yanaongeza hadhi ya mji wetu.
ReplyDeleteI dont think hii ni solution kwa tatizo la usafiri Dar. Just short time solution.
ReplyDelete