Serikali imekubaliana na mifuko ya hifadhi ya jamii kuanza utekelezaji wa ujenzi wa viwanda nchini ili
kuhakikisha kuwa adhma ya Tanzania ya kufikia uchumi wa viwanda inafanikiwa ifikapo mwaka
2020.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli aliyeitaka mifuko hiyo kuwekeza
katika ujenzi wa viwanda nchini.
Akizungumza mara baada ya kikao cha pamoja baina ya Serikali na mifuko hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Ulemavu, Jenister Mhagama alisema Serikali
imekusudia kuhakikisha uanzishwaji wa viwanda unaanza haraka na kuongeza fursa za ajira nchini.
Mhagama alisema kuwa mali ghafi na nguvu kazi ya kutosha zipo hapa nchini hivyo hakuna sababu
ya kuchelewa kuanza, ambapo Serikali imepanga hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016,
utekelezaji wa adhma hiyo inaanza kuonekana machoni mwa Watanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya hifadhi ya Jamii
(SSRA)alisema, Irene Isaka alisema ni agizo hilo limekuja katika wakati mwafaka kwa kuzingatia
kuwa kwa mifuko ya Hifadhi ya jamii imekusudia kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali ya
awamu ya tano inayosisitiza kuijenga Tanzania kupitia uchumi wa viwanda.
Kwa mujibu wa Isaka alisema kuwa kanuni na mifumo ya mifuko hiyo inaruhusu suala la uwekezaji
katika viwanda ama kwa njia ya ubia au ya hati fungani au kutoa mikopo kwa wanotaka kuwekeza
katika viwanda.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt, Adelhelm Meru alisema
uwekezaji katika viwanda ni suala ambalo linawashirikisha wadau wengi zikiwemo wizara za Kilimo,
Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya malighafi za viwandani, Elimu kwa ajili ya ujuzi wa watu wa kufanya kazi
viwandani na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya nishati ya kuendesha viwanda.
“Kwa kuangalia raslimali tulizo nazo tumewaomba wadau waanze na viwanda ambavyo vilikuwepo
lakini kwa sasa havifanyi kazi kama vile Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC), General Tyre, NARCO na
Kiwanda cha Viwadudu cha Kibaha, alisema Dr. Meru na kuongeza kuwa malighafi za viwanda hivi
zinapatikana hapa nchini.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha mashauriano ya pamoja baina ya Serikali na Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii kuhusu adhma ya ujenzi wa viwanda nchini wakifuatilia kwa makini kikao
hicho kilichoitishwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na
Ulemavu). Kikao hicho kilifanyika leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Bw. Adam
Mayingu na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Bw.
William Urio wakifuatilia kikao cha pamoja baina ya mifuko ya hifadhi ya jamii na Serikali
kuhusu adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu), Mhe. Jenister
Mhagama akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuhusu adhma ya
utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kahyarara (katikati)
akizungumza katika kikao baina ya mifuho ya hifadhi ya jamii na Serikali kilichozungumzia
adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Urio na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
Kujipanga kufufua uchumi wa viwanda kuende sambamba na kuhamasisha maendeleo kote nchini. Kwa sababu wale wanaoishi maisha ya ujima bila kuwa na mabati, viti, vitanda, vitasa, umeme na vifaa vyake, maji,ujenzi wa sementi, rangi za nyumba, vyoo vya kisasa, hawatasaidia kuinua uchumi kama consumers au wanunuzi wa vifaa vya viwandani wakiachwa nyuma. Kuwekeza kwenye kuinua maisha ya wananchi na uwezo wao wa kutumia bidhaa zilizoko sokoni na zinazotoka viwandani kutaongeza pato la taifa na ajira za muda mrefu.
ReplyDeleteThe mdudu, Asantenii sana wanachi tupo pamoja na hapa kazi2 jengeni viwanda vya nguvu ili wananchi wengi wapate kazi humo viwandani
ReplyDeleteNi jambo zuri sana hili la Mifuko kuwekeza kwenye viwanda ila kwa sasa sidhani kama wana uwezo na utaalamu wa kuchanganua miradi ipi inafaa na italeta tija kwahio ningeshauri wajikite kwenye kuwekeza kwente taasisi zenye utaalamu na uwezo huo kama Benki ya Kilimo, Benki ya Maendeleo na Mercantile Exchange.
ReplyDelete