Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema katika futari aliyoiandaa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye makazi yake jijini Dares salaam Juni 10, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi (kushoto) na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Siro katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam , Simon Siro katika futari aliyoiandaa kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania , Abdallah Buelembo katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Juni 10, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
MAJALIWA: UHABA WA SUKARI KUMALIZIKA NCHINI.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini ambapo jumla ya tani 20,000 zilisambazwa jana katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema shehena nyingine ya tani 35,000 inatarajiwa kusambazwa hivi karibuni katika kanda zote nchini hivyo amewataka wafanyabiashara watakapoipokea kuiuza kwa wananchi bila ya kuificha na bei isizidi shilingi 2,200.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana jioni ( Ijumaa, Juni 10, 2016) wakati akizungumza na Masheikh na Viongozi wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Dar es Salaam alipowaalika katika futari aliyoiandaa nyumbani kwake.
Amesema tayari viwanda vimeanza kufunguliwa na tani 300 zilizotoka katika kiwanda cha Sukari cha Kagera zitasambazwa katika wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu, Uvinza na Kigoma ili kutosheleza maeneo hayo.
Hata hivyo amewataka Maofisa Biashara katika Halmashauri zote nchini kuendelea kufanya ufuatiliaji katika maduka ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana na hakuna mfanyabiashara atakayeificha.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara kote nchini kutopandisha bei za vyakula katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza kuhusu tabia za baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa hasa vyakula katika kipindi hiki cha mfungo amewataka kumuogopa Mwenyezi Mungu kwa sababu kitendo hicho kinawapa wafungaji wakati mgumu.
“Kufunga Ramadhani si jambo la anasa, si matashi binafsi bali ni jambo la kiimani hivyo tusipandishe bei ya bidhaa kwa lengo la kuwaadhibu Waislam kwa sababu tu wamefunga.
“Katika Quran surat Baqarah aya ya 183 inasema kwamba enyi mlioamin imefaradhishwa kwenu kufunga kama walivyoamrishwa kufunga kwa waliopita kabla yenu ili muwe wachamungu, hivyo hatuna budi kufunga” alisisitiza.
Alisema tabia hiyo si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo kwa wafanyabiashara kuamua kupandisha bei hivyo aliwataka waiache kwani Serikali haitawavumilia na atakayethubutu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...