Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Ngabaganga Taraba amekabidhi vifaa mbalimbali kwa wanafunzi waliounguliwa bweni katika Shule ya Sekondari Shinyanga wilayani humo.
Taraba aliwashukuru wanafunzi hao kwa jitihada za kuuzima moto huo ambao ungeweza kusambaa katika mabweni mengine na kuharibu mali na vifaa vingine.
Aliwataka kusahau machungu yaliyotokea na badala yake ajikite katika kusoma kwa bidii ili waje kuwa kwani machozi yao yamefutwa baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.
Akiwasilisha taarifa ya tukio hilo, Kaimu Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kishapu, Paul Kasanda alisema moto huo uliotokea Julai 11, 2016 uliunguza vifaa na mali zote kwenye bweni hilo.
Alisema Mkuu wa wilaya na timu ya watumishi walifika shuleni hapo na kufanya tathmini ya hasara na mahitaji ya wanafunzi waliounguliwa na hivyo kuchukua hatua ya kuwapatia misaada.
Misaada iliyotolewa ni pamoja na magodoro yenye thamani y ash. Milioni 1.8, mashuka 72 sh. 648,000, na vifaa vingine yakiwemo mavazi vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh. laki saba.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Ngabaganga Taraba akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shinyanga waliounguliwa na bweni ambapo mali mbalimbali ziliteketea kwa moto.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Ngabaganga Taraba akigawa vifaa kwa mmoja wa wanafunzi 11 waliounguliwa katika bweni shuleni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Ngabaganga Taraba akigawa vifaa kwa mwanafunzi aliyeathirika na tukio la kuungua kwa moja ya mabweni shuleni hapo. Wengine katikati ni Kaimu Afisa Elimu Sekondari wilayani humo, Paul Kasanda.
Wanafunzi wakifurahia vifaa walivyokabidhiwa na Mkuu wa Wilaya.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...