Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wakati wa uzinduzi wa huduma za CHF iliyoboreshwa (ICHF) iliyoratibiwa na Shirika la Kimataifa la PHARMA ACCESS. Tukio hilo limefanyika mapema leo Julai 11.2016, Wilayani Babati katika mji wa Bashnet.
Baadhi ya watendaji wa Serikali katika Miji na Vijiji pamoja na maafisa Ustawi wa jamii wakiwa mbele baada ya Dk. Kigwangalla kuwaita mbele haapo na kisha kuwapa angalizo la miezi sita wawe wamesimamia vizuri mradi huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mapema leo Julai 11.2016 amezindua rasmi huduma za Afya za CHF iliyoboreshwa katika Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara ambapo amewaagiza watendaji wa Serikali wakiwemo Maafisa wa Ustawi wa Jamii,
Walimu, Watendaji wa Serikali Kata, vijiji na Maafisa Maendeleo kuhakikisha wanasimamia zoezi la kuhamasisha wananchi wanachangamkia furza za kujiunga na mfuko huo haraka katika kuboresha afya za wananchi wote.
Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema hayo katika Mji wa Bashnet ambao upo katika Wilaya hiyo ya Babati, Mkoani hapa.
“Natoa maagizo kwa watendaji wote kuhakikisha munausaidia kutoa taarifa sahihi ili wananchi wapate kujiunga na huduma hii ya ICHF. Na pia sitaki kusikia kama wananchi waliojiunga na hudua hii ya CHF iliyoboreshwa wanakosa dawa ama huduma huko Mahospitali ama kituo chochote cha Afya, ikibainika Serikali itachukua hatua kali.
Aidha. Watendaji wote wakiwemo muliopo kwa jamii huko, muhakikishe munahamasisha na kuwaingiza wananchi wote kwenye mfuko huu. Natoa miezi sita kwa Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo, Watendaji wa Serikali za Vijiji, na Maafisa wengine wote nitakaporejea hapa baada ya miezi sita nikute huduma hii ya CHF iliyoboreshwa imekuwa kubwa na wananchi wengi wamejiunga na endapo kwenye eneo lako limekuwa la mwisho basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yako” alieleza Dk. Kigwangalla.
Katika tukio hilo, lililofanyika katika viwanja vya minada vya Bashnet-Babati, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukabidhi vitendea kazi ikiwemo Pikipiki kadhaa kwa watendaji ambao watakuwa wakitoa huduma hizo za CHF iliyoboreshwa, ambapo pia alikabidhi kadi kwa wanachama waliojiunga papo hapo.
Katika shughuli hizo ambazo zimeratibiwa na Shirika la Kimataifa la PHARMA ACCESS, pia Dk. Kigwangalla aliweza kuzindua kituo cha Afya kilichofanyiwa ukarabati mkubwa na shirika hilo katika kituo cha Afya cha Dongobesh.
Mbali na kuzindua kituo hicho cha Afya cha Dongobesh kilichofanyiwa ukarabati mkubwa na PHARMA ACCESS, Dk. Kigwangalla pia aliweza kuweka jiwe la msingi katika jengo la chumba cha upasuaji wa kituo hicho ambapo alitoa miezi sita kwa Afisa Tawala wa Wilaya kuhakikisha wanakamilisha jengo hilo la chumba cha upasuaji.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...