Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye Kaunda suti akitembezwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited Bw. Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya .(Picha E.madafa, D.Nyembe)
Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited Bw. Derick ambaye kampuni yake ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla aneo ambalo litachimbwa madini hayo.
Ramani ya mradi.
Na Mwandishi wetu, Mbeya
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali
ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza
Ndege na computer. Mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na
kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza
Afrika
Mkurugenzi
wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5
kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria
zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika
mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji
mapema mwaka 2018.
Mkuu wa
mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa sanjali na
kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa viongozi na wananchi kwa
kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi. Aidha amewataka wananchi na
viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo
uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali
kwa hslmashauri na serikali kuu.
Pia
amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7
zilizokuwa na upungufu wa madawati Hata hivyo Gereza la Songwe mkoani Mbeya
linatalaji kuvunjwa na kuhamishiwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini
hayo adhimu ya duniani ya niobium baada ya madini hayo kugundulika kuwepo
karibu na maeneo ya gereza hilo la Songwe.
Kwa
mujibu wa taarifa za wataalam zinadai kuwa madini ya mgodi huo huchanganywa na
metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi bomba la kupitishia mafuta
sanjali na metali zake kutumika katika injini za ndege ili kuzuia mitambo yake
kutopata joto kali.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...