Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela usiku wa kuamkia leo alishiriki katika kuzima moto uliounguza bweni wanaloishi watoto yatima katika kituo cha Mgongo mjini Iringa. Moto huo ilioanza kwa hitalafu ya umeme umeteketeza mabweni matatu na kuunguza mali za watoto hao ikiwemo nguo, amadaftari ba magodoro.
Kikosi cha zimamoto chini ya Mrakibu Komba kilifanya kazi ya ziada kuzuia moto huo usieneee majengo mengine. Wananchi wa eneo la Mgongo wamefanya kazi kubwa wakisaidiana na jeshi la zima moto.
Akizungumza na wananchi Mh Kasesela ameahidi kuomba wahisani pia kuangalia uwezekano wa kuwasaidia waathirika wa janga hili la moto. Inakadiriwa watoto zaidi ya 45 wameathirika na moto huu ingawaje hamna majeruhi hata mmoja.
"Nilipata taarifa nikiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ikabidi niache nije mara moja nafurahi kuona tumefanikiwa kuzima moto ingawaje umeleta madhara makubwa.
"Pongezi ziwandee jeshi la Zimamoto pamoja na changamoto walifanikiwa kuzima moto huo" aliesema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wawilaya huyo alikutana na watoto na kuwapa matumaini serikali ipo pamoja nao. Serikali ya Wilaya ya irnga inawaomba wadau wajitokeze kusaidia watoto hawa mahitaji makubwa ikiwa ni magodoro, blanketi na nguo hasa kipindi hiki cha baridi.
DC Kasesela akizungumza na watoto ambao vitu vyao vimeungua .
Mkuu wa wilaya akishirikiana na zimamot kuwapanga wananchi
DC Kasesela akishirikiana na zimamoto kuwapanga wananchi
DC Kasesela akishirikiana na zimamoto kuzima moto huo






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...