Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Marwa Petro (kushoto) akielezea majukumu ya Wizara mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kutoka kulia, mbele) mara Naibu Katibu Mkuu alipotembelea banda la Wizara kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Musa Chowo (kushoto) akieleza gridi ya Taifa inavyofanya kazi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto)
Mtaalam kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) akieleza jinsi shughuli za ukaguzi wa madini zinavyofanyika nchini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( wa kwanza kushoto) mara alipotembelea banda la TMAA.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (katikati) akioneshwa jinsi majiko yanayotumia nishati mbadala yanavyofanya kazi na Afisa Masoko kutoka Kampuni ya Envotec Services Limited Salama Sudi (kulia) ambao ni mdau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...